ROZARI YA BIKIRA MARIA
Matendo ya Furaha
Matendo ya Furaha I
1. Kupashwa habari Bikira Maria kuwa atakuwa Mama wa Mungu. Maria alisema ndio kwa mpango wa Mungu, na hapa alimpata Yesu Kristo; ingawa, hakujua jambo hilo litakamilikaje. Tunawaombea wamama wote wawe na ujasiri wa kupokea zawadi ya uhai (Lk 1:26-38).
2. Bikira Maria alimtembelea Elizabethi. Binamu yake kumjulia hali kwani alikuwa amepata ujauzito katika uzee wake. Ingawaje, Maria alihitaji msaada yeye aliamua kumsaidia Elizabeth. Tunawaombea wababa wote wawe na moyo wa huruma na upendo kwa wake na watoto wao (Lk 1:39-45).
3. Yesu Kristo alizaliwa na Bikira Maria. Katika sehemu duni sana. Wazazi wa Yesu walimpenda sana mtoto wao (Lk 2:5-7). Tunawaombea wazazi wote wawe na upendo kwa watoto wao.
4. Yesu alipelekwa hekaluni. Kama sheria ilivyoagiza kuwa mtoto akiwa na umri wa siku 40 apelekwe hekaluni. Tunawaombea wazazi wawe tayari kuwatoa watoto wao kama sadaka machoni pa Mungu kwa kuwabatiza mapema na kulea miito yao (Lk 2:22-24).
5. Maria na Yosefu wanamkuta Yesu Hekaluni. Yesu alipokuwa na miaka 12 alienda hekaluni na huko alipotea na wazazi wake walimpata baada ya siku 3. Tunamuomba Mungu awajalie imani wale wote waliopoteza imani kwa Yesu Kristo na waliopoteza watoto (Lk 2:41-52).
Matendo ya Furaha II
1. Kupashwa Bikira Maria habari kuwa atakuwa Mama wa Mungu; haikuwa mpango wa awali wa Bikira Maria. Maria hakutegemea kwani hata hakujua mwanaume kabisa, pamoja na mshtuko huo Maria alikubali mtoto kwa moyo wote. Bikira Maria uwe mfano wa kuigwa kwa wamama wote wanaogopa uzazi. Wawe tayari kupokea uhai.
2. Bikira Maria kumtembelea Elizabethi; ambaye alipata mimba katika uzee wake, Elizabeth alihofu sana kuwa katika umri wake huo atawezaje, kumlelea mtoto wake. Elizabeth hakuwa mwenyewe, familia yake ilimzunguka na kumfariji. Bikira Maria uwaombee wamama wote wanaoishi katika hofu na mashaka makubwa.
3. Kuzaliwa kwa Yesu Kristo. Tunajiuliza kuwa kwa nini Yesu akubali kuzaliwa na mwanadamu na kuishi maisha ya shida na mwisho afe kifo cha aibu msalabani? Bikira Maria tunaomba uwaombee wale wote wasiotambua thamani ya uhai na maisha.
4. Yesu anapelekwa hekaluni kuitii torati. Bikira Maria tunaomba uwaombee wazazi wote wawe watiifu kwa mpango wa Mungu ambaye ndiye mpaji wa uhai.
5. Maria na Yosefu wanamkuta Yesu hekaluni. Kuna wakati walimpoteza Yesu ila walihangaika kumtafuta. Bikira Maria ombea familia ambazo muda mwingine zinasahau nafasi ya Mungu katika maisha yao hasa wakati wa misukosuko.
Matendo ya Furaha III
1. Kupashwa Bikira Maria habari kuwa atakuwa Mama wa Mungu kunaingia mashaka baada ya Malaika kumwambia Maria kuwa atakuwa mama wa Mungu. Maria aliuliza. “JAMBO HILI LITAWEZEKANAJE?” Leo hii kuna akina mama wanapata mashaka makubwa sana wanapoambiwa na daktari kuwa ni wajawazito. Tumuombe Mungu awape wamama ujasiri wa kupokea uhai bila mashaka na hofu.
2. Bikira Maria kumtembelea Elizabethi lilikuwa tendo la kindugu. Bikira Maria alienda kumsaidia binamu yake ili asijisikie mpweke katika siku zake za kujifungua. Leo hii kuna wajawazito wengi wanapata kishawishi cha kutoa mimba kwa sababu ya kukosa msaada. Tuwaombee wajawazito ili wapate msaada kutoka kwa watu mbalimbali.
3. Yesu anazaliwa Bethlehemu katika h ri la ng’ mbe, embeni yake alikuwa Maria, Y sefu, Malaika na wanyama. Baadae wachungaji na Mamajusi. Mfalme wa amani na mshauri wa ajabu amezaliwa katika mazingira duni sana. Kila mtoto anayezaliwa ni muujiza usiojali umetokea wapi na kwa muda gani. Tuwaombee wanaume na wanawake watambue thamani kubwa ya kila uhai Mungu aliowajalia.
4. Yesu kutolewa hekaluni siku 40 baada ya kuzaliwa kwake ni kutekeleza torati, anatolewa kama sadaka kwa Mungu, ni jambo jema sana wazazi kuwatoa watoto wao kama sadaka kwa Mungu. Tuwaombee wazazi wawatolee watoto wao kwa Mungu na Maria.
5. Maria na Yosefu wanamkuta Yesu hekaluni. Yesu akiwa na miaka 12 alipelekwa hekaluni, alipotea na wazazi wake walimwona baada ya siku tatu. Tuwaombee wazazi ili daima wamsikilize Mungu na kufuata maagizo yake katika maisha yao na kuthamini wito wa watoto wao.
Matendo ya Mwanga
Matendo ya Mwanga I
1. Yesu anabatizwa mtoni Yordani. Yesu anabatizwa na Yohane ndugu yake, Yesu hakuhitaji kubatizwa kwa sababu hakuwa na dhambi, lakini anakubali ubatizo ili atusafishe sisi. Bikira Maria wakumbushe wazazi wote umuhimu wa kuwabatiza watoto wao na kuwapa malezi ya kikristo. Ubatizo wa Roho Mtakatifu watufanya wana wapendwa wa Mungu (Lk 3:21-22).
2. Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Yesu hakuruhusu maharusi kupata aibu kwa kukosa divai. Maria muombe mwanao Yesu kama ulivyofanya katika harusi ya Kana ili wale wote wanaojiandaa kuoa na kuolewa wawe na moyo wa uchaji, waishi pamoja katika shida na raha hadi kifo kiwatenganishe, washika Agano la ndoa kitakatifu (Yn 2:1-11).
3. Yesu anatangaza ufalme wa Mungu. Daima Yesu aliwafundisha watu kuacha njia zao mbaya na kumgeukia Mungu. Alituonyesha kuwa lengo letu kuu ni kuufikia ufalme wa Mungu. Maria tukumbushe amri za Mungu, na uwasaidie wanaotunga sheria hapa duniani walinde uhai. Hotuba ya Mlimani yanatueleza Ufalme wa Mungu unayoleta furaha ya kweli (Mt 5:1-7:29).
4. Yesu anageuka sura mlimani Tabor. Petro, Yakobo na Yohane walikuwepo na Yesu, walishuhudia utukufu wa Yesu. Mavazi ya Yesu yalikuwa meupe sana. Maria tuombee kwa mwanao ili tuiendee Sakramenti ya upatanisho na kugeuza namna za maisha yetu (Mt 17:1-13).
5. Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. Yesu aliwaamuru wanafunzi wake kuendelea kuiadhimisha hii Sakramenti mpaka mwisho wa nyakati. Kwenye karamu ya mwisho Yesu alifanya tendo lililotokea ijumaa kuu. Maria ulikaa chini ya msalaba siku ya ijumaa kuu. Tufundishe namna ya kushiriki vizuri misa takatifu (Lk 22:19-23).
Matendo ya Mwanga II
1. Yesu anabatizwa mtoni Yordani. Yesu alipokubali kuwa mwanadamu na kubatizwa kama sisi alianza utume wake rasmi hapa duniani, alichukua mateso, maumivu na kukataliwa kwa wanadamu, Bikira Maria tuombee kwa Yesu mwanao, waombee wamama walea peke wote, ili wawe na nguvu na ujasiri wa kuendelea na maisha yao wakimtegemea Mungu.
2. Muujiza wa maji kuwa divai huko Kana. Baada ya divai kuisha katika harusi, Bikira Maria hakubabaika kwa sababu alijua mwanae atamsaidia katika hilo. Maria waombee wamama wote wanaoogopa kujifungua watoto wagonjwa na wenye ulemavu, wape moyo wa kuyapokea yote kadiri ya mpango wa Mungu.
3. Yesu anatangaza ufalme wa Mungu. Yesu aliwaambia wafuasi wake wawe kama watoto wadogo ili waurithi ufalme wa Mungu. Maria tuombee kwa mwanao ili tuwajali wale wadhaifu hapa duniani ambao ndio watakaourithi ufalme wa Mungu.
4. Yesu anageuka sura mlimani Tabor. Yesu aliwaonyesha wanafunzi wake utukufu alionao, hii iliwaogopesha sana wanafunzi wake. Bikira Maria tusaidie daima tuishi maisha ya ukweli.
5. Yesu anaweka Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. Yesu alitaka kuimarisha muungano na ushirikiano kati ya Mungu na wanadamu. Bikira Maria waombee wanawake wote wasiotambua kwamba kwa kuleta uhai duniani wanashiriki muujiza mkubwa wa Mungu.
Matendo ya Mwanga III
1. Ubatizo wa Yesu mtoni Yordani. Hapo ikasikika sauti toka mbinguni ikisema, “huyu ni mwanangu m endwa, niliye endezwa naye” (Mk 1:11). Ubatiz ni akramenti ya kwanza kabisa, watoto wadogo wanapobatizwa Mungu anawaambia maneno haya aliyomwambia Yesu. Mungu anapendezwa na kila mwanadamu. Tuwaombee wazazi wote watambue kwamba watoto wao wanapendwa sana na Mungu.
2. Yesu anageuza maji kuwa divai huko Kana. Yesu na wanafunzi wake walialikwa katika harusi huk Kana, lakini divai iliisha, Bikira Maria alili na hil na akawaambia “l l te atakal waambia fanyeni” (Yn 2:5). Wak wazazi wengi wenye matatizo hasa ya kupata watoto, tunawaombea ili wamkimbilie Yesu kitulizo halisi na kujifunza kupokea kwa imani mapenzi ya Mungu juu ya maisha yao.
3. Yesu anatangaza Ufalme wa Mungu. Yesu alionyesha upendo wake kwa watu wote. Kila mmoja ana nafasi ya kipekee sana katika ufalme wa Mungu. Ni jukumu la kila mmoja kuheshimu uhai kwani unatoka kwa Mungu na thamani yake ni kubwa sana. Tuwaombee wote wanaoshiriki katika kuuharibu uhai ili wafanye mabadiliko ya ndani kabisa.
4. Yesu anageuka sura mlimani Tabor. Petro, Yakobo na Yohane waliona utukufu wa Mungu kwa Yesu Krist ale mlimani. Na Mungu mwenyewe alisema “huyu ni mwanangu m endwa” (Mk 9:7). Tunamuomba Mungu ili nasi tuuone wa utukufu wake katika maisha yetu.
5. Kuwekwa kwa Sakramenti ya Ekaristi Takatifu. Yesu alichukua mkate na kusema “Twaeni mle” na akachukua kik mbe cha divai akasema “twaeni mnywe” ili ku ambana na uovu juu ya uhai ni lazima kula na kunywa Mwili na Damu ya Yesu Kristo. Tumuombe Mungu ili kwa Mwili na Damu ya Yesu Kristo uhai wa mwanadamu uthaminiwe na kutunzwa na watu wote.
Matendo ya Uchungu
Matendo ya Uchungu I
1. Yesu anatoka jasho la damu. Yesu aliteseka kwa sababu alizichukua dhambi zetu ikiwemo dhambi ya kutoa mimba. Bikira Maria wasaidie wamama waliotenda dhambi hii nguvu na ujasiri wa kutubu (Lk 22:44).
2. Yesu anachapwa mijeledi. Yesu alimwaga damu yake kwa uchungu mkubwa. Bikira Maria wasaidie madaktari wanaomwaga damu ya watoto wachanga kubadilisha njia za maisha yao na kumgeukia Mungu (Mk 15:15).
3. Yesu anavikwa taji la miiba. Maaskari wa kirumi walimdhihaki na kumtukana Yesu. Bikira Maria waombee wababa ambao hawawalindi watoto wao katika hatari ya kifo (Mk 15:17).
4. Yesu anabeba msalaba. Watu walimpiga na kumtemea mate akibeba msalaba wake kuelekea kalvari. Katika safari hiyo ngumu wapo pia waliomsaidia na kumfariji. Bikira Maria wasaidie wamama walio wapweke kupata watu wa kuwafariji na kuwasaidia (Lk 23:24-25).
5. Yesu anakufa msalabani. Alikubali kifo cha aibu ili atukomboe kutoka utumwa wa dhambi.Bikira Maria waombee msamaha wale wote wanaoelemewa na dhambi ya utoaji mimba (Lk 23:44-46).
Matendo ya Uchungu II
1. Yesu anatoka jasho la damu. Yesu kabla ya kuteseka alipata mashaka na woga ila mwishoni alikubaliana na mapenzi ya Mungu. Bikira Maria waombee wanandoa ambao hawana watoto ili wakabidhi maisha yao kwa Mungu na wakubaliane na mapenzi ya Mungu.
2. Yesu anapigwa mijeledi. Yesu alikufa kwa unyofu wake na akamkomboa mwanadamu mdhambi. Alichukua dhambi za mwanadamu hata za kutoa uhai wa mwanadamu.
3. Yesu anavikwa taji la miiba. Walimtukana na kumtemea mate ingawa, hakuwa na kosa lolote. Bikira Maria uziombee roho za watoto waliotolewa mimba.
4. Yesu anabeba msalaba. Aliubeba msalaba wake hadi Kalvari hakuutupa msalaba wake. Bikira Maria waombee wazazi wasiowakubali watoto wenye vilema na magonjwa, wawapokee na kuwatunza.
5. Yesu anakufa msalabani. Mama Maria aliumia sana kuona mwanae anakata roho msalabani. Bikira Maria waombee wazazi wanaoumia baada ya kuwapoteza watoto wao.
Matendo ya Uchungu III
1. Yesu anatoka jasho la damu. “Inukeni msali msije, mkaingia majaribuni” (Lk 22:46). Yesu anaonyesha umuhimu wa kudumu katika sala. Baadhi ya watu wanaamua kutoa mimba kwa starehe zao wenyewe. Tumuombe Mungu abadili mioyo ya watu ili wajue thamani ya uhai na kuutunza.
2. Yesu anapigwa mijeledi. Yesu aliumizwa sana kwa mijeledi kila tunapotenda dhambi tunamchapa Yesu mijeledi. Tumuombe Mungu atusamehe dhambi zote hasa zile za kutojali uhai.
3. Yesu anavikwa taji la miiba. Maaskari wanampiga na kumtemea huku wakisema “salamu mfalme wa wayahudi” (Mk 15:18). Tuwe tayari kwani tukifanya mamb mema na yanayompendeza Mungu tutateseka. Tumuombe Mungu ili wafuasi wake wawe na uvumilivu na unyenyekevu.
4. Yesu anachukua msalaba. Yesu alibeba udhaifu, mateso, maumivu, tamaa, makosa na kila kitu kinachotuelemea. Njiani alionana na watu waliomdhihaki lakini wengine walimsaidia na kumpa faraja. Katika maisha yetu kama Wakristo tunakutana na hawa watu wote.
5. Yesu anakufa msalabani. Yesu alisema “Yametimia” (Yn 19:30). Na akait a R h yake. Utume wetu ni kutoa maisha yetu kwa ajili ya wengine. Mapambano yetu juu ya kuulinda uhai yabarikiwe na tuzidi kuupigania uhai na thamani yake itunzwe.
Matendo ya Utukufu
Matendo ya Utukufu I
1. Yesu anafufuka. Siku tatu baada ta kifo chake, Yesu alifufuka. Kwa kuwa mtiifu kwa Mungu, Yesu aliishinda dhambi, kifo na shetani. Bikira Maria waombee ulinzi watoto wote na uwaepushe na utoaji mimba (Yoh 20:8-9).
2. Yesu anapaa mbinguni. Siku arobaini baada ya ufufuko wake Yesu alipaa Mbinguni. Ameketi mkono wa kuume wa Baba. Bikira Maria tunaomba uziombee familia zote ambazo wajawazito wapo ili thamani ya uhai ionekane (Mdo. 1:9).
3. Roho Mtakatifu anawashukia Mitume. Roho Mtakatifu analifundisha na kulisimamia Kanisa hadi mwisho. Bikira Maria tunaomba utuombee tuwe na ujasiri wa kutangaza utetezi wa uhai (Mdo. 2:1-4).
4. Bikira Maria anapalizwa Mbinguni. Huyu ni mwanadamu wa kwanza ambaye ameunganika kabisa na Mungu mwili na roho. Bikira Maria utuombee sisi wakosefu sasa na saa ya kufa kwetu.
5. Bikira Maria anawekwa Malkia Mbinguni. Malkia huyu ni wa kwanza katika viumbe kuinuliwa juu kabisa Mbinguni. Bikira Maria tuombee tuwe watu wa huduma.
Matendo ya Utukufu II
1. Ufufuko wa Yesu. Yesu ni tumaini letu kwani ameshinda kifo na ametuonyesha njia ya wokovu. Kila tunapoulinda uhai tunausogelea wokovu wetu. Bikira Maria tuombee katika njia yetu hii tudumu katika kuutetea uhai.
2. Yesu anapaa mbinguni. Wanafunzi wake walikuwa wakitazama mbinguni mara wakasikia sauti, “enyi watu wa Galilaya mb na mwatazama mbinguni? Yesu mliyemu na akienda zake mbinguni, ndivy atakavy rudi” (Md 1:9-11). Bikira Maria tuombee kwa Mungu ili daima tulinde uhai wa hawa walio dhaifu.
3. Kushuka kwa Roho Mtakatifu. Mungu ametutumia Roho wake Mtakatifu ili awe Mfariji wa imani yetu na kutusaidia kuchagua kati ya mema na mabaya kila siku. Maria, uwaombee watu wote ambao wanachangia kulinda maisha, na hata kwa matendo madogo kabisa.
4. Bikira Maria anapalizwa Mbinguni. Mama huyu alishuhudia mazuri na mabaya yaliyompata Yesu. Bikira Maria uwe mfano wa wazazi wa leo, waweze kubeba furaha na machungu ya kuwa wazazi.
5. Bikira Maria anawekwa kuwa Malkia Mbinguni. Tujifunze kukubali mapenzi ya Mungu katika maisha yetu. Tujifunze kumuita Bikira Maria ili atufundishe kuyapokea mapenzi ya Mungu katika maisha yetu.
Matendo ya Utukufu III
1. Yesu anafufuka. Sasa kifo sio mwisho kwani Yesu ameshinda kifo (Yn 16:33). Yesu anawaambia wanafunzi wake “amani iwe nanyi” (Yn 20:19). Wazazi wengi wako katika mahangaiko na hawana amani maishani mwao. Tumuombe Yesu mfufuka ili awasaidie na kuwapatia amani ya kweli.
2. Yesu anapaa Mbinguni. Yesu aliwaambia Mitume wake “enendeni mkawafanye mataifa y te wanafunzi wangu” (Mt 28:19). Daima tusichoke kutangaza Injili ya kutetea uhai kwa watu wote.
3. Roho Mtakatifu anawashukia mitume. Huyu ni Roho wa uhai hivyo tuwaombee wale wote wanaotaka kumvaa roho wa mauti na kumuacha Roho wa uhai.
4. Bikira Maria anapalizwa Mbinguni. Mama huyu daima yuko na Yesu, pia ni Mama yetu hivyo kamwe tusijione kama tuko peke yetu, daima wamama wajawazito wamuite ili awasaidie katika mahangaiko yao. Daima tumuombe Mungu ili mapenzi yake yatimie katika maisha yetu.
5. Bikira Maria anawekwa Malkia Mbinguni. Mama huyu daima yuko tayari kutusaidia. Mt.Benard anasema “hakuna aliyekimbilia kwa Bikira Maria na akak sa msaada”. Tumuombe Mungu awaangazie wazazi wote kuukimbilia msaada wa mama Bikira Maria.