Kuasili Kiroho Mtoto Ambaye Hajazaliwa Bado

“Taifa linaloua watoto wake halina kesho ” – Mt. Yohane Paulo II

Mt. Yohane Paulo II

Mwisho wa mwaka 1919 daktari wa magojwa ya wanawake na mtaalamu wa uzazi huko Wadowice (Poland), alimwambia Emilia Wojtyła kuwa ujauzito wake ulikuwa hatarini na kwamba mtoto anaweza kuzaliwa tu kwa gharama ya maisha yake. Katika hali hii, alipendekeza kutoa mimba, kwa maoni yake, mwanamke huyo asingeweza kuishi wakati wa kujifungua. Kwa Emilia mwenye umri miaka 36 alijisikia mwenye huzuni kubwa, kwa sababu miaka mitatu iliyopita alipoteza mtoto wa kike. Sasa daktari alikuwa anapendekeza kifo cha mtoto wa pili. Mama Emilia akaamua, kwamba hata kama atakufa, ni lazima mtoto azaliwe.
Mtoto yule alizaliwa tarehe 18 mwezi wa tano mwaka 1920 na mama yake aliishi takriban miaka tisa. Yule mtoto alibatizwa kwa jina la Karol Józef Wojtyła, ambaye alichaguliwa baadae kuwa Baba Mtakatifu, Yohane Paulo II.

Injili ya maisha (Evangelium vitae)

Mnamo wa mwaka 1975 Baba Mtakatifu Yohane Paulo II aliandika: “Injili ya maisha ni kiini cha ujumbe wa Yesu Kristo. Kanisa linaipokea kila siku kwa upendo ili kuitangaza kwa uaminifu na kwa ujasiri kama habari njema kwa watu wa kila kizazi na utamaduni. Habari ya kuzaliwa kwa mtoto ilitangazwa kama habari ya kufurahisha: ‘Tazama, ninawatangazia furaha kuu ambayo itakayowashirikisha watu wote: leo, katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi’ (Lk 2: 10-11). Kwa sababu ya siri ya Neno la Mungu aliyefanyika mwili (taz. Yoh 1:14), kila mtu amekabidhiwa huduma na mama Kanisa. Kwa sababu hii, kila tishio kwa utu na maisha ya mwanadamu hutikisa sana moyo wa Kanisa, linagusa kiini cha imani yake katika mwili wa Mwana wa Mungu na Mkombozi na linahimiza Kanisa kutekeleza utume wake wa kutangaza Injili ya masiha kwa ulimwengu wote na kwa viumbe vyote (Mk 16:15). Tangazo hili linakuwa muhimu sana leo wakati woga unasababishwa na vitisho vinavyoongezeka na kubwa zaidi kwa maisha ya watu na mataifa, hasa wanyonge na wasio na ulinzi” (Evangelium vitae namba 1 na 3).

MWALIKO

Sisi hatutaki kukaa kimya katika hali hii ngumu sana. Kila mwaka duniani kote wanaouawa ni zaidi ya milioni hamsini. Hatutajua kamwe walikuwa na vipaji gani, wangetusidia katika maisha yetu ya hapa duniani; mfano Mt. Yohane Paulo II. Watoto ambao bado tumboni mwa mama zao hawawezi kusema chochote. Kwa hiyo sisi ndio tuna nafasi ya kuwatetea ili wapate kuzaliwa na kupata maisha.
Ufanyeje? Umwasili kiroho mtoto moja ambaye hajazaliwa bado. Maana yake nini? Umwombee kila siku kwa muda wa miezi tisa kwa sala, ambayo imependekezwa hapo chini na tendo moja la Rozari Takatifu utakalochagua. Inatosha? Ndiyo. Kwa njia hii utakuwa mzazi wa kiroho wa mtoto, ambaye hujui taifa lake wala kabila lake, wala lugha yake.
Somo wa zoezi hili ni Mitume wa Huruma – Mtakatifu Yohane Paulo II, Mtakatifu Faustina na Mwenyeheri Pd. Mikaeli Sopoćko, kwa sababu ni tendo la huruma pia. Hao watatu watakusaidia ukijitolea kwa moyo wa dhati kumwasili mtoto kiroho. Karibu tujenge umoja katika tukio hili la kusikitisha.

Kuasili kiroho mtoto ambaye hajazaliwa bado ni nini? (KuKi)

Kuasili kiroho ni nadhiri anayoweka mtu kwa lengo la kumuombea mtoto ambaye hajazaliwa bado na wazazi wake, ili apate usalama tumboni mwa mama yake na baadaye maisha mazuri baada ya kuzaliwa. Jina la mtoto anayeombewa linafahamika na Mungu.
Maana ya tendo hili ni kusali kila siku kwa miezi tisa; sala maalumu, na fungu moja la rozari takatifu. Unaweza pia kuongeza matendo ya huruma na mazoezi ya kiroho kama kufunga au kusoma maandiko matakatifu na mazoezi mengine ya kiroho. Majitoleo haya yanaendana na kuwaelimisha watu wengine kujiunga na zoezi hili la kuasili mtoto kiroho.

Malengo matatu ya kuasili mtoto kiroho  

Kuwahamasisha wazazi kusali ili waweze kupokea zawadi ya uhai ambayo Mungu anawashirikisha katika familia.

Kuwaelimisha watu wote hasa vijana na watoto juu ya ukuaji na maendeleo ya mtoto tumboni mwa mama.

Kuwapatia msaada akina mama wahitaji, ambao ni wajawazito au wana watoto wachanga.

Maana ya Nadhiri

Nadhiri ni ahadi mtu anayomuwekea Mungu kufanya au kuacha kufanya jambo fulani katika maisha. Malengo ya ahadi hiyo ni ufalme wa Mungu. Kwa mfano mtu hawezi kuweka nadhiri ya kushiriki Misa takatifu kila Dominika kwa sababu sheria ya Mungu na ya Kanisa yatutaka tufanye hivyo. Nadhiri huwekwa kwa uhuru kamili wa mtu. Nadhiri yaweza kuwa kujikatalia mambo fulani kama kilevi na anasa nyingine.
Nadhiri ya kuasili mtoto kiroho ni kujitolea kusali kumuombea mtoto aliyetungwa mimba, na wazazi wake ili uhai wa mtoto huyu ulindwe na kuheshimiwa siku zote toka kutungwa mimba. Anayefanya tendo hili anatakiwa kusali fungu moja la rozari kila siku kwa miezi tisa, na kumtolea Mungu sadaka kwa ajili ya msamaha wa dhambi ya utoaji mimba.
Ahadi hii ni hai na ina nguvu pale inapowekwa kwa uhuru kamili wa mtu binafsi. Kila aliyeweka nadhiri hii lazima awe makini na kutekeleza kile alichomuahidi Mungu ili kupata mastahili ya nadhiri hii, kushindwa kuishi nadhiri hii kwa makusudi na uzembe ni dhambi mbele ya Mwenyezi Mungu. Nadhiri hii hudumu kwa miezi tisa, muda huu ndio makadirio ya muda ambao mtoto hukaa tumboni mwa mama yake.
Nadhiri: kama ahadi kwa Mungu zina thamani kubwa sana kwa anayeziweka. Nadhiri zikifuatwa vizuri humuongezea Yule aliyeziweka nguvu ya kuishi maisha ya maadili na kumpendeza Mungu. Pia nadhiri huimarisha uhusiano kati ya mtu na Mungu, pamoja na kwamba wapo ambao hupinga nadhiri kwa kigezo kwamba hufunga uhuru wa mwanadamu lakini nadhiri ni tendo la hiari kabisa analolifanya mtu baada ya tafakari ya kina. Hivyo katika nadhiri kuna uhuru kamili usio na ubinafsi.

Nani anaweza kuasili mtoto?

Mtu anayeasili mtoto kiroho anatenda tendo la sadaka na heshima kwa Mungu. Ingawa mtu huyu anaweza asimuone huyo mtoto, wala kumkumbatia, wala kumgusa, ila analinda maisha ya mtoto huyo aliyemuasili. Kwa kutamka maneno ya sala kwa moyo kabisa mtu aliyeasili mtoto anamuomba Yesu awaguse wazazi wa mtoto aliyeko hatarini, kubadili mtazamo wao na kutunza uhai wa mtoto. Pia hii itasaidia wazazi kutambua kuwa familia ni jumuiya ya asili ambayo yahitaji upendo na makuzi ya kipekee kila siku. Ni vizuri vijana, watoto wa shule na wanandoa wakifanya zoezi hili la kuasili mtoto kiroho. Kama wakichukua hatua ya kuikomboa roho ya mtoto hata wasiomfahamu, wao watakuwa makini zaidi kwa watoto wao. Kuasili mtoto kiroho kama tendo la sala binafsi hutengeneza kikundi cha sala ambapo wahusika huweka ahadi kanisani, kipindi cha Misa au Masifu ya jioni ya sherehe fulani ya kanisa 4 (mfano. Sherehe ya Kupashwa Habari Bikira Maria au siku za kawaida). Pia yawezekana ahadi hizi zikawekwa katika mazingira mengine kama nyumbani kwa wazee na wagonjwa ambao hawawezi kufika kanisani. Hawa waweza kuweka ahadi zao mbele ya Msalaba au sanamu ya Bikira Maria na baadaye kumpa padri taarifa juu ya ahadi hii.

Namna ya kuweka ahadi za kuasili mtoto kiroho

Nakusifu Mungu Baba. Bwana wa mbingu na nchi, kwa sababu mambo haya umewaficha wenye hekima na akili, ukawafunulia watoto wachanga. (Mt 11,25; Lk 10,21)
Bikira Maria Mama wa Mungu, Malaika na Watakatifu wote. Kwa kutambua umuhimu wa kulinda uhai wa mtoto ambaye hajazaliwa bado, Mimi ………………………….. naahidi kuanzia leo (katika sherehe/sikukuu ya …………….) kuasili kiroho mtoto ambaye jina lake linafahamika na Mungu tu, naahidi kusali kwa miezi tisa kila siku ya maisha ya mtoto huyo kwa ajili ya ukombozi wa maisha yake na kwa ajili ya ustawi wa maisha yake atakapozaliwa. Nitasali fungu moja la rozari ya Bikira Maria na Sala ya kila Siku, ambayo leo nitaisali kwa mara ya kwanza na kwa hiari nitafanya mazoezi ya kiroho.

SALA YA KILA SIKU

Ee Bwana Yesu Kristo, nakuomba kwa mastahili ya maombezi ya mama yako Bikira Maria aliyekuzaa kwa upendo mkuu na ya Mtakatifu Yosefu, baba yako mlishi aliyekulea baada ya kuzaliwa kwako, uyasikilize maombi yangu. Ninakuja mbele yako kukuomba umlinde mwanangu wa kiroho, ambaye hajazaliwa bado na ambaye uhai wake uko hatarini kuangamizwa! Nakusihi, Ee Bwana, uwape wazazi wa mtoto huyu moyo wa upendo na uthabiti wa kuutunza uhai uliomjalia. Amina

Utakapoanza zoezi hili tafadhali ujaze fomu hii:

6 + 6 =